Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la Iran Press limeripoti kuwa, mashindano ya kijeshi ya majeshi ya dunia katika fani ya "Masters of Arms" yameanza tangu tarehe 22 mwezi huu na yanaendelea hadi Septemba 3 mwaka huu katika mji wa Isfahan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Moja ya malengo ya duru ya sita ya mashindano hayo ya kijeshi ya majeshi ya dunia huko Isfahan ni kuimarisha amani, urafiki na kuzidisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya Iran, Russia, Vietnam na Uzbekistan.
Wanajeshi wanaoshiriki mashindano hayo tajwa katika fani ya Masters of Arms wanatumia silaha mbalimbali nzito na nyepesi za kimaidani, ulinzi wa anga na silaha binafsi, makombora ya Katyusha n.k.
342/